Mchepuko Adaiwa Kuua MKE wa Mtu



Mwili wa Teddy Malya (31) mkazi wa Ilboru Kisiwani, Arumeru mkoani hapa, umekutwa umetupwa kwenye shamba la migomba huku ukiwa mtupu na baadhi ya majeraha mwilini akidaiwa kuuawa na hawara wake (mchepuko).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo, picha: mtandao
Mwili huo ulikutwa eneo hilo jana majira ya saa 2:30 asubuhi na wapiti njia na kuuchukua kwenda kuhifadhiwa katika eneo la kutunzia maiti ndani ya Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

Mwanamke huyo anadaiwa kutoonekana siku moja kabla ya mwili huo kugundulika na wapitanjia ukiwa kwenye shamba hilo huku majani yakiwa yamevurugika .

Taarifa za wakazi wa eneo hilo, zimedai kwamba marehemu alikuwa na uhusiano wa siri na mwanamume nje ya ndoa ambaye anadaiwa kutekeleza mauaji hayo. Inadaiwa kuwa mwanamume huyo alikuwa na ugomvi akimtuhumu mwanamke huyo kutoa ujauzito wake, jambo ambalo mume wa marehemu alikanusha.

Mme wa marehemu, Richard Lanyuni (42) alisema aligundua mke wake kuuawa baada ya kupokea taarifa za wapitanjia kuwa kuna mtu amelala kwenye shamba la migomba ndipo alipofika na kukuta ni mkewe akiwa amepoteza maisha.


Akihojiwa na waandishi wa habari, Lanyuni alisema mkewe ambaye hufanya biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya mbege, hakuonekana kurejea nyumbani muda wa kawaida na ilipotimu majira ya saa saba usiku, aliamua kulala ndipo kesho yake alipata taarifa za kuuawa.

"Mke wangu anafanya biashara ya kuuza pombe za kienyeji siku hiyo hakurejea nyumbani lakini nimeambiwa siku ya tukio alionekana akiwa na kijana mmoja anayefahamika.kwa jina moja la Baraka," alisema Lanyuni.

“Kuhusu mke wangu kuwa na uhusiano na mwanamume huyo, siwezi kujua ila hakuwa na ujauzito. Naomba vipimo vya kitaalamu vifanyike kujua kama kweli alikuwa na ujauzito maana ana shughuli zake mimi siwezi kumchunguza sana," alisema.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo, alisema Jeshi la Polisi linamshikilia mtu mmoja (jina limehidhadiwa kwa ajili ya uchunguzi) mwenye jinsia ya kiume kwa tuhuma za kumuua mwanamke huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilkiroriki, Emmanuel Lazaro, mtuhumiwa alikuwa anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu enzi za uhai wake.

Mwenyekiti huyo alisema Mallya alikamatwa kutokana na baadhi ya nguo zake na viatu kukutwa eneo la tukio, jambo ambalo waliamini anahusika na mauaji hayo.

"Huyo jamaa alikamatwa kwenye nyumba mojawapo hapo mtaani amejificha na kilichosababisha ni baada ya viatu vyake pamoja na nguo kukutwa eneo la tukio," alisema Lazaro.


Alisema jambo lingine lililowatia wasiwasi ni baada ya kumkuta mtuhumiwa akiwa na majeraha ya meno sehemu mbalimbali za mwili wake, kitendo kinachoashiria walikuwa na purukushani na marehemu kabla ya mauti kumfika.

Lazaro alisema mallya kabla ya mauti kumfika, alionekana akiwa na mtuhumiwa katika baa mojawapo mtaani wakinywa pombe kabla ya kupatikana akiwa ameshafariki dunia.

"Tukio hili limetushtua sana sisi Kama wakazi wa huu mtaa Kka kuwa si la kawaida lakini tumeukuta mwili wa marehemu ukiwa hauna nguo na inaonekana alibakwa kabla ya kuuwawa," alisema Lazaro.

Baadhi ya majira wanadai kwamba mtuhumiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu wakidai kwamba mtuhumiwa alikasirishwa na hatua ya marehemu kudai kutoa ujauzito wake jambo ambalo liliibua sintofahamu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad