Mchezaji wa Zamani wa Simba Afunguka "Amerudi Nyuma, Haikuwa Sahihi yeye Kurudi Tena Simba"



Kiungo fundi wa zamani wa Simba, Shekhan Rashid amevunja ukimya baada ya kurejea kwa Clatous Chama kwenye klabu ya Simba msimu huu wa dirisha dogo.
Chama alijiunga na Berkane RBS ya Morocco, Agosti mwaka jana, baada ya Simba kumuuza, ambako amecheza kwa muda mfupi kabla ya kurejea tena Simba hivi karibuni.

Akizungumza jana, Shekhan anayeishi nchini Sweden alisema kwa Chama kuondoka Simba na kisha kurejea si jambo baya kwa kuwa amerudi kwenye timu anayoipenda.

“Ingawa kwa mtazamo wangu naona ni kama amerudi nyuma, haikuwa sahihi yeye kurudi tena Simba, tayari alishatoka na kwa alipokuwa amefika alipaswa kwenda mbali zaidi kisoka,” alisema Shekhan.

Alisema licha ya kumpenda mchezaji huyo na kufurahia uwepo wake Simba, ila kisoka, anaona Chama hakufanya uamuzi sahihi kurejea Simba.

“Alitakiwa aende mbele zaidi, tungemuona aidha kwenye timu za Ulaya baada ya kutoka Morocco, binafsi naona kama kurudi kwake Simba haukuwa uamuzi sahihi katika muendelezo wake soka.

“Japo nampenda na ninaona ana mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba, ni mchezaji mwenye kiwango bora, ila kurudi Simba ni kama amejirudisha nyuma badala ya kwenda mbele,” alisema.

Akizungumzia baadhi ya wanasoka nchini kushindwa kukopi maisha ya mpira nje ya nchi, Shekhan aliyewahi kucheza soka la kulipwa enzi zake alisema changamoto kubwa inatokana na wengi wao kutoyakuali maisha tofauti na waliyoyazoea nchini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad