Mgonjwa Ashikiliwa na Polisi kwa Tuhuma za Kuiba GARI la Wagonjwa na Kusepa Nalo



Mgonjwa mwenye umri wa miaka 40, aliyejulikana kwa jina la Saminu Sa’idu, amezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kwa kutuhumiwa kuiba gari ya wagonjwa hospitali aliyokua amelazwa.


Mshukiwa huyo wa wizi anaripotiwa kukamatwa na kuanikwa hadharani na kamanda wa polisi wa jimbo la Kano nchini Nigeria.


Watumiaji wa mitandao wameduwazwa na tukio hilo wakijiuliza ni nini ambacho mgonjwa huyo alitaka kufanya na gari hilo.


Kwa mujibu wa gazeti la Leadership, Sa’idu alikamatwa baada ya polisi kufahamishwa, kuwa gari la wagonjwa liliibwa katika kijiji kimoja cha Dawakin Tofa.



Inataarifiwa kuwa mshukiwa huyo aliiba ‘ambulance’ ya Halmashauri ya Serikali ya Mtaa wa Ungogo huko nchini Nigeria.


Kulingana na msemaji wa polisi wa jimbo hilo, ASP Lawan Shiisu, mshukiwa huyo alikamatwa siku moja baada ya taarifa za kupotea kwa gari hiyo kuwafikia na alikamatwa katika kijiji cha Takwasa, Babura.


Aliongeza kuwa polisi walipokea taarifa kuwa kuna gari ya wagonjwa ambayo haina namba za usajili inaonekana mitaani na ilipatikana ikiwa na mihadarati.



“Baada ya kupokea taarifa hiyo, makachero wa Kanya Babba, tarafa ya Babura, walichukua hatua na kufanikiwa kulinasa gari hilo katika kijiji cha Takwasa mnamo Desemba 11, saa 08.00, likiendeshwa na mkazi wa Halmashauri ya Daura, Jimbo la Katsina,” ilisoma sehemu ya taarifa hiyo, kama ilivyoripotiwa na Shirika la Habari la Nigeria.

Hizo ni harakati za watu wanaochelewesha maendeleo ya wananchi kwa maeneo tofauti ulimwenguni bila kujali afya ya jamii yake na huduma za kijamii zinavyowasaidia kimaendeleo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad