Mkenya kuachiliwa kutoka Guantanamo Bay baada ya miaka 15



 
Guled Hassan Duran (kushoto) na Mohammed Abdul Malik Bajabu Picha: CNN
Mkenya Mohammed Malik Bajabu na Guled Hassan Duran, raia wa Somalia, wanatazamiwa kuachiliwa kutoka katika gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba. 

Wawili hao wamekuwa katika gereza la Marekani huko Guantanamo Bay, Cuba, kwa zaidi ya muongo mmoja. 

Bajabu amekuwa ikishikiliwa katika gereza hilo tangu 2007 huku Duran akizuiliwa tangu 2006. Kulingana na CNN, wawili hao waliruhusiwa kuachiliwa, kulingana na stakabadhi za umma. 


Maamuzi hayo yanajiri wakati gereza hilo likiadhimisha miaka 20 wiki hii tangu lilipofunguliwa chini ya utawala wa George W. Bush. 

CNN iliripoti kwamba Rais Joe Biden alisema hadharani kwamba anataka kufunga gereza hilo na Baraza la Usalama la Kitaifa linapitia ukaguzi wa gereza hilo "ili kubaini njia mwafaka ya hatma yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad