Msemaji mpya Simba aanza vijembe



MKUU mpya wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa timu ya Simba nchini Tanzania, Ahmed Ally ameanza majukumu yake kwa ‘kuwazodoa’ watani zao Yanga kwamba wataambulia patupu katika Kombe la Mapinduzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni baada ya leo asubuhi Jumatatu, tarehe 3 Januari 2022, Simba imemtangaza Ahmed kushika nafasi hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Haji Manara ambaye alitimikia Yanga.

Ahmed amejiunga na Simba akitokea Azam Media alikohudumu kwa miaka mitatu. Alijiunga na Azam akitokea Sahara Media Limited (Star TV na Redio Free Afrika).

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ahmed ameweka picha akiwa safarini kwenda Zanzibar na Simba kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyoanza jana ambapo bingwa mtetezi ni mtani wao Yanga, aliyechukua kombe hilo mwaka jana kwa kuwafunga Simba.


 
Picha hiyo imeambatana na maneno, “Safari kuelekea Zanzibar. Safari kwenda kuchukua Kombe la Mapinduzi.”

“Yess ni rahisi na inawezekana tupo tayari. Tunafahamu wengine hili ndo Kombe lao pekee la kujivunia hivyo tunalichukua Ili tuwakumbushe kuwa sisi ni Wakubwa kwao.”


Amesema, “saa 8:20 Insha Allah, nitakua Forodhani na baadae saa 11:15 jioni nitahudhuria mazoezi ya kwanza ya timu katika Uwanja wa Mao tse Tung.”

Aidha, Ahmed ameshukuru alikotoka akisema, “niwashukuru watazamaji wa Azam TV niliokuwa nao kwa kipindi cha miaka mitatu hadi leo naanza kuitumikia taasisi kubwa hapa nchini, timu ya ndoto yangu.”

“Imekuwa faraja kwangu kuitumia Simba,” amesema alipohojiwa moja kwa moja na Azam TV leo mchana akiwa Zanzibar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad