Web

Mtoto wa Profesa Jay, Wa Babalevo Watusua



FAMILIA za mastaa wawili Bongo Profesa Jay na Baba Levo zimegubikwa na furaha baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka na watoto wao kung’ara kwa kupata daraja la kwanza.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Profesa Jay amempongeza binti yake huyo kwa kuandika;

“Matokeo Form Four. Lisa Joseph Haule –division one point 10. Congratulations to my beautiful daughter @l.i.s.a.h_profjize. Safari ndiyo kwanza inaanza, keep your head up. Pia hongera sana mama mzaa chema @mke_ wa_profjize kwa miongozo na malezi bora kwa mwanetu…”

Kwa upande wa Baba Levo, pamoja na mwanawe Levo kufanikiwa kupata division one ya pointi 9 katika matokeo ya kidato cha pili, lakini amesema hampi zawadi mpaka apate division one ya pointi 7.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad