Mtu Wangu Kuwa Makini..Mvua Kubwa Kuendelea Kunyesha, TMA Wataadharisha



MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la kuendelea kunyesha mvua katika maeneo ya ukanda wa Pwani ikiwemo Da es Salaam na maeneo mengine nchini. Aidha, imetoa ufafanuzi wa mvua na upepo mkali uliotokea juzi usiku kuwa ulitokana na mwenendo wa hali ya hewa.

Mchambuzi wa hali ya hewa katika mamlaka hiyo, Joyce Makwata alisema mvua kubwa itaendelea kunyesha katika maeneo ya ukanda wa Pwani na kusini mwa nchi. Alisema mvua za msimu wa masika zinaendelea katika maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka na zitaendelea katika siku chache mpaka mwishoni mwa wiki ya nne ya mwezi huu.

Alisema inatarajiwa kuwepo na upungufu wa mvua Pwani ya kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki na ukanda wa Ziwa Victoria . “Lakini pia katika maeneo ya kusini mwa nchi yanayopata mvua mara moja kwa mwaka ambapo kwa kawaida Huanza Novemba na Aprili mwaka unaofuata inatarajia kuendelea kwani ni mvua za msimu,” alisema Makwata.

Alitoa ufafanuzi wa mwenendo wa hali ya hewa na vipindi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo vilivyotokea hivi karibuni ikiwemo mvua zinazoambatana na upepo mkali katika maeneo ya Pwani ya kaskazini na kusini na baadhi ya maeneo ya nchini. Alisema hali hiyo ilitokana na uwepo wa mawingu mazito yanayosababisha mvua ambapo kwa kawaida uwepo wa mvua zinazosababishwa na mawingu hayo huambatana na vipindi vya upepo mkali.


Makwata alishauri wananchi kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua kama kuharibika kwa miundombinu na kuzingirwa na maji na kuathiri biashara katika maeneo ya wazi . “Wananchi wanashauriwa kuendelea kufutilia taarifa za hali ya hewa za kila siku ili kujikinga na hali mbaya ya hewa ikiwemo mvua kubwa,” alisisitiza

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad