Mwalimu Ampa Mama wa Mpenzi Wake Figo Yake, Asalitiwa na Kuachwa Baada ya Mwezi



MWALIMU mmoja aitwaye Uziel Martinez ameteka hisia za watu baada ya kuweka video zake katika mtandao wa TikTok akilia kwa uchungu baada ya kuchangia figo kwa mama wa mpenzi wake na kuishia kusalitiwa baada ya mpenzi wake kuolewa na mwanaume mwingine baada ya mwezi mmoja tangu atoe figo.

Tukio hilo la Martínez ambaye ni mwalimu nchini Mexico katika eneo la Baja California, limewagusa wengi huku wengi wao wakidai kuwa mwanadada huyo aliyemuacha mwezi mmoja tu baada ya ku-donate figo yake kwa mama mkwe hana utu hata kidogo.

Video hiyo ambayo imesambaa duniani kote na kwenye vyombo mbalimbali vya habari, baadhi ya watu wamemshauri Martinez kutafuta mwanamke sahihi aachane na huyo naliyeamua kuumiza moyo wake.

Martinez amewahakikishia watu hao kuwa yuko vizuri kimwili na kiakili na sasa anaendelea kujiuguza ili kupona jeraha alilofanyiwa upasuaji kutoa figo hiyo kumpa mama mkwe.


Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad