Mwanafunzi wa Sekondari Avae Hata Sare ya Shule ya Msingi




Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, ameendelea kusisitiza kwamba wakuu wa shule kutoweka vikwazo kwa wanafunzi wataokuwa hawana sare za shule badala yake wawaruhusu kuingia darasani hata na sare zao waliuzokuwa wanavaa shule ya msingi.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januri 6, 2021, wakati akitoa tamkoa maalum kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuanza masomo Januari 17, huku akimshukuru Rais Samia kwa kuwezesha ukamilikaji wa madarasa 12,000 nchini.

“Nimewaita hapa kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma kuhusu hali ya uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Awali, Darasa la Kwanza na mandalizi ya kuwapokea wa Kidato cha Kwanza kabla ya kufungua Shule za Msingi na Sekondari tarehe 17 Januari, 2022.

“Takwimu za maoteo ya uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Awali zinaonesha kuwa jumla ya Wanafunzi 1,363, 834 (Wavulana 676,028 na Wasichana 687,806) wanatarajiwa kuandikishwa ikilinganishwa na idadi ya Wanafunzi 1,198,564 (Wavulana 604,995 na Wasichana 593, 569) walioandikishwa 2021, Idadi hii inajumuisha Wanafunzi wenye mahitaji maalum 6,376 wakiwemo Wavulana 3,277 na Wasichana 3,099.


 
“Uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Awali ulianza Novemba, 2021 na unaendelea, hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2021 jumla ya Wanafunzi 488,780 wa Darasa la Awali wakiwemo Wasichana 247,003 na Wavulana 241,777 sawa na asilimia 35.93 ya Wanafunzi wote wanaotarajiwa kuandikishwa Darasa la Awali, waliandikishwa katika Shule za Serikali, idadi hii, inajumuisha Wanafunzi wenye mahitaji maalum 1,232 ambapo Wasichana ni 642 na Wavulana 590.

“Kama ni mwanafunzi wa sekondari anaweza akatumia sare yake aliyokuwa anavaa shule ya msingi wakati mzazi anatafuta fedha au akavaa tu t-shirt na sketi yake nzuri akaenda darasani, wazazi pia waangalie joining instruction (maelekezo ya kujiunga na shule) inasema nini kwa sababu kuna vitu vingi ambavyo havina hata umuhimu, jamani tuondoe vikwazo.

“Kwa upande wa Kidato cha Kwanza mwaka 2022 jumla ya Wanafunzi 907,803 wakiwemo Wavulana 439,836 na Wasichana 467,967 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2021 ikilinganishwa na Wanafunzi 833,872 waliojiunga kidato cha kwanza 2021, Wanafunzi hao wanatarajiwa kuanza masomo tarehe 17 Januari, 2022 na orodha yao tayari imekwishatolewa ikionesha Shule wanazotakiwa kusoma.


“Uchambuzi unaonesha kuwa Mikoa mitano yenye matarajio ya kupokea Wanafunzi wengi zaidi kwa Kidato cha Kwanza ni Dar es Salaam (78,738), Mwanza (68,725), Kagera (50,735), Mara (48,855) na Morogoro (48,515).

“Jumla ya Wanafunzi wanaotarajiwa kuandikishwa Shuleni kwa mwaka wa masomo 2022 ili waanze masomo Januari, 2022 ni 3,853,460, hii ikiwa ni Wanafunzi wa Darasa la Awali 1,363,834; Darasa la Kwanza 1,581,823 na Kidato cha Kwanza 907,803, ikilinganishwa na Wanafunzi 3,631,715 wakiwemo Wanafunzi 1,198,564 wa Darasa la Awali, Wanafunzi 1,549,279 wa Darasa la Kwanza na Wanafunzi 883,872 wa Kidato cha Kwanza 2021.

“Takwimu za maoteo ya uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Kwanza zinaonesha kuwa jumla ya Wanafunzi 1,581,823 (Wavulana 788,620 na Wasichana 793,203) wanatarajia kuandikishwa ikilinganishwa na Wanafunzi 1,549,279 wakiwemo Wavulana 775,339 na Wasichana 773,940 walioandikishwa 2021, idadi hii inajumuisha Wanafunzi wenye mahitaji maalum 10,645 wanaotarajiwa kuandikishwa wakiwemo Wavulana 5,724 na Wasichana 4,921.

“Uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Kwanza ulianza Novemba, 2021 na unaendelea, hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2021 jumla ya Wanafunzi 663,486 wakiwemo Wavulana 329,538 na Wasichana 333,948 sawa na asilimia (41.94%) ya Wanafunxi walikuwa wameandikishwa katika shule za Serikali, idadi hii, inajumuisha Wanafunzi wenye mahitaji maalum 1,601 wakiwemo Wavulana 819 na Wasichana 782


 
“Uchambuzi wa takwimu hizo unaonesha kuwa, Mikoa 05 inaongoza kwa uandikishaji ambayo ni Manyara (70.95%), Njombe (62.06%), Singida (54.23%), Dodoma (54.23%) na Lindi (52.46%), aidha mikoa, ambayo takwimu za uandikishaji zipo chini ni pamoja na Rukwa (18.62%), Katavi (18.83%), Shinyanga (26%), Mwanza (26.26%) na Mtwara (27.98%).

“Uchambuzi wa takwimu hizo unaonesha kuwa, Mikoa 05 ambayo inaongoza kwa uandikishaji ni Manyara (57.99%), Mara (49.37%), Njombe (49.00%), Tanga (47.85%) na Mbeya (46.99%), Mikoa 05 ambayo takwimu za uandikishaji zipo chini ni Mwanza (21.17%), Dar es Salaam (20.44%), Mtwara (19.52%), Rukwa (17.33%) na Katavi (8.39%), takwimu hizo zinaonesha kuwa, Mkoa wa Manyara pekee ndio una uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Awali zaidi ya asilimia 50,” amesema Waziri Ummy.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad