Mwanamke mwenye umri wa miaka 20 kutoka Madagascar anashikiliwa na polisi baada ya kuhisiwa kujifungua kwenye ndege ya Air Mauritius na kumtupa mtoto huyo kwenye ‘dustbin’ iliyopo kwenye vyoo vya ndege.
Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam huko Mauritius walimkuta mtoto mchanga jinsia ya kiume ambaye alikuwa ametelekezwa kwenye pipa la kuhifadhia taka (dustbin) katika ndege hiyo.
Hata hivyo Mwanamke anayeshukiwa kuwa mama wa mtoto huyo ambaye awali alikana hadi alipofanyiwa uchunguzi wa kimatibabu ambao ulithibitisha kuwa alikuwa amejifungua. Mwanamke huyo aliwekwa chini ya uangalizi wa polisi katika hospitali ya Umma Kwa matibabu na imeelezwa kwamba yeye na mtoto wanaendelea vizuri.