Mwanamke wa Guatemala aliyezuiliwa katika kambi ya kijeshi na kubakwa kwa siku 25





Ilikuwa Jumapili ya kawaida kwa Paulina Ixtapá.

Alikuwa na miaka 19 na alikuwa akitembea na mama yake kuelekea katika manispaa ya Rabinal, mji uliopo eneo la kati mwa Guatemala, karibu kilomita 100 kutoka jiji kuu la nchi hiyo.

"Watu fulani walikwenda kwa mama yangu na kusema 'tunataka kuongea na binti yako,'" Paulina aliambia BBC Mundo, akikumbuka kilichotokea mchana huo wa mwaka 1983 ambao ulibadilisha maisha yake.

Wanaume hao walikuwa wanachama wa Doria za Ulinzi wa Raia (PAC): kundi la walinzi lililobuniwa na serikali ya kijeshi ya Guatemala wakati huo kwa lengo la kutaka kujumuisha raia katika masuala ya ulinzi wa nchi dhidi ya ghasia kutoka kwa makundi ya wapiganaji wa mrengo wa kushoto.

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Rigoberta Menchú aliandamana na wanawake wa Achí kutoka Rabinal mwanzoni mwa kesi yao.
Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Rigoberta Menchú aliandamana na wanawake wa Achí kutoka Rabinal mwanzoni mwa kesi yao.

Leo karibu miaka 40, baada ya kisa hicho wanachama watano wa Rabinal PAC wanakabiliwa na mchakato wa kihistoria wa mahakama kwa madai ya ubakaji wa kimfumo dhidi ya wanawake 36 wa Achí kutoka manispaa hiyo ya Mayan. Paulina ni mmoja wa wahasiriw hao wa ubakaji.

"Utakutana na mume wako baadae"
Mchana huo wa Jumapili, wanaume waliokuwa wakifanya doria, na ambao walikuwa wamevalia sare, walimuelekeza Paulina katika kambi ya kijeshi katika eneo hilo. Hakuwa mwanamke pekee hapo.

"Nilipofika kambini waliniuliza, 'Mume wako yuko wapi?' Niliwaambia kuwa sina mume na hapo wakanijibu: 'Utakutana na mume wako baadae.'

Kulingana na mwanamke huyo, wanaume hao walimuuliza kuhusu madai ya mahusiano ya kimapenzi aliyokuwa nayo "na kapteni Juan," lakini akawaelezea kuwa ameondoka kitambo kidogo.

Jibu hilo inaonekana sio kile wanaume hao wa kushika doria walitaka kusikia.

Paulina anasema mmoja wa wanaume hao alimshika shingo kwa nguvu na kusema: " Sasa utatuambia ni watu gani wanaokuja nawe usiku."


Kulingana na Lucía Xiloj, wakili wa waathiriwa 29 wa kesi ya wanawake wa Achí kutoka Rabinal, unyanyasaji huo wa kingono ulifanywa kati ya mwaka 1981 na 1985, ndani ya mfumo wa mzozo wa ndani wa silaha huko Guatemala.

" Wanawake hawa waliwekwa kizuizini kinyume cha sheria na kupelekwa katika kambi yaa kijeshi ambapo walikuwa wahasiriwa wa ubakaji wa hadharaniwa mara kwa mara, alisema Xiloj.

Wanachamawa PAC sehemu muhimu ya juhudi za serikali ya kijeshi ya wakati huo kukomesha waasi wa mrengo wa kushoto, na unyanyasaji wa kijinsia ulitumiwa kama silaha ya vita ili kujua nani kati ya watu alikuwa wa upande gani.

Hii imesababisha mawakili wa waathiriwa kuiwajibisha serikali ya Guatemala kwa "kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa wanawake wanaishi maisha yasiyo na unyanyasaji wa kijinsia."

Hata hivyo, bado haijabainika ikiwa serikali itajumuishwa katika kesi kama mhusika anayewajibika.

Ubakaji na uhamisho
Paulina anasema kutoka usiku huo wa mwaka 1983, na saa 24 zilizofuata, alilazimishwa kusalia katika kambi ya kijeshi. Na anaongeza kuwa wakati huo kila usiku, alikuwa muathirika wa vitendo vya kuvunja moyo na dhulma za kingono.

Wanawake wa Achí wa Rabinal wakisubiri kuanza kwa kesi yao
Chanzo cha picha, Getty Images



"Wakati wa kuzuiliwa kwa siku 25 katika kambi hiyo, walinibaka kila usiku. Na waliponiachilia, nilitoka nikiwa mgonjwa na daima, nikiteswa [...] waliniambia kuwa wakiniona katika jamii, wataniua. mara moja."

Kutokana na hali hiyo, Paulina aliamua wenda mji mkuu ili kutoroka jamii. Na ijapokuwa alirejea baadaye , anasema mchakato wa uponaji ulikuwa mgumu na wa mateso.

"Kwangu ilikuwa vigumu sana. IIlikuwa ngumu kwa sababu kando na kunibaka pia waliwaua watoto kadhaa. Walioba mifugo wetu . Walichoma nyumba zetu. Na mahali nilipokuwa naishi , nilikusalia na nguo chache za kubdalisha."

Hii ndio sababu kesi iliyoanza Januari 5 ni muhimu sana kwa wanawake wa Rabinal.

Kupitia taarifa iliyotolewa Septemba mwaka 2021, twanawake hao walisema: "Tumekuwa tukisubiri kwa miaka 40 kutendewa haki kutokana na unyanyasaji wa kijinsia na maovu tuliyopata wakati wa mzozo wa ndani wa silaha huko Rabinal, Baja Verapaz."


"Tumekuwa tukingojea haki kwa miaka 40," wasema wanawake wa Achí wa Rabinal.

Kana kwamba miaka 40 ya kungoja haitoshi, kesi iliyopangwa kuanza Januari 4 ilicheleweshwa kwa saa 24 za ziada.

Wakikabiliwa na changamoto ya kucheleweshwa upya kwa kesi hiyo, baadhi ya wanawake wa Achí walifanya sherehe ya Mayan mbele ya Mahakama ya Juu zaidi.

Hatimaye kesi hiyo ilianza kusikilizwa Jumatano, Januari 5, na taarifa kutoka kwa upande wa mashtaka na utetezi, na washtakiwa kufuatilia mchakato kwa njia ya kiteknolojia.

Sasa, wahasiriwa wanatumai kuwa masaibu yao yatajulikana na haki itatendeka. Angalau ndivyo Paulina anavyotarajia.

"Natafuta haki, na watarudisha kila kitu walichoiba. Lakini walichokifanya kinaniumiza."
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad