Mwanzilishi wa Mtandao wa Match.com Aliachwa na Mke Wake Baada ya Kukutana na Mwanaume Mwingine Kupitia Mtandao huo Alioanzisha Mumewe


Mwaka 1993 Gary Kremen ambaye ni Founder wa Mtandao wa Match. Com unaowakutanisha Watu pamoja na kuanzisha mapenzi (Dating App), aliachwa na Mpenzi wake baada ya Mpenzi wake huyo kukutana na Mwanaume mwingine kwenye mtandao huo wa Match. Com na wakajikuta wamependana hadi kuamua kuachana na Gary.

"Nilipoona hakuna namna ya kuwakutanisha Watu kwa urahisi nikaanzisha App, Mke wangu pia nikamruhusu awe na akaunti huko, sikutegemea kitu nilichokitengeneza mwenyewe kitakuwa chanzo cha kuniachanisha na Mpenzi wangu niliumia sana lakini sijutii maana ilionesha kwamba App imepokelewa vizuri Mtaani"

Kwa sasa Match.com ni miongoni mwa Mitandao 500 mikubwa Duniani ukiwa na Watumiaji 21,575,000 lakini mafanikio haya yalianza kwa Muanzilishi kukubali kuibiwa Mpenzi.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad