“Hakuna siku Mtanzania mmoja mmoja atagongewa mlango kuwa nchi yake ilikopa, haitatokea, hivi ni vitu vya kitaasisi na inalipwa katika mapato ya serikali.
“Haitatokea Mtanzania atafuatwa atoe ng’ombe kwa kuwa nchi yake ina deni la serikali.
“Pia si jambo la kiungwana kusema kuwa Rais amekaa miezi tisa amekopa, Rais hakopi ni serikali, hili siyo jambo la familia ni jambo la serikali.
“Ndiyo maana katika miezi tisa aliyokaa amekuwa akilipa madeni hata ya nyuma kila mwezi, Waziri wa Fedha," - Mwigulu Nchemba wakati Rais Samia akipokea taarifa ya utekelezaji wa matumizi ya fedha zA UVIKO -19, leo Jumanne, Ikulu, Dar es Salaam.