Mtangazaji Mwijaku
Kwa mara nyingine mwijaku amejitokeza na kueleza kuwa ubunifu wa Wasafi wa muziki unaendelea kudidimia kila uchao.
Mwijaku ambaye ni mtangazi wa kituo kimoja cha radio nchini Tanzani ameeleza kuwa wakati umewadia ambapo Wasafi inafaa kuanza kuangazia lebo hio kwani mambo si sawa.
Alieleza kuwa Wasafi imesaini wasanii wengi ambao wameanza kuonekana kuishiwa na ubunifu jambo ambalo limeanza kulemaza kazi ya lebo hio
Alisema wakati Wasafi ilikuwa ikianzia ilikuwa na uwezo mkubwa wa kuuza tiketi nyingi kuliko sasa jambo ambalo linaonyesha upetepetevu ulioko kwenye lebo hio.
Wasanii ambao wamesainiwa na Lebo ya Wasafi ni ; Zuchu, Ravyaan, Lava lava na Queen Darling.
Mwaka huu wasanii ambao wameachilia wimbo na lebo ya hio , ni wawili tu, ambao ni Zuchu na Ravyaan.
Mwijaku ameeleza kuwa msanii ambaye anajituma zaidi ni Diamond kuhakikisha lebo hio inaendelea kwa kufanya collabo na wasanii sifika ndani na nje ya nchi.
Isitoshe alitoa mfano kwamba wasanii ambao hawako kwenye lebo yeyote wameanza kuonekana kufanya vizur.