Mwili wa DESMOND Tutu Wayeyushwa




Mwili wa aliyekuwa mpambanaji maarufu wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Desmond Tutu uliagwa Jumamosi katika mazishi ya kiserikali kwenye Kanisa Kuu la St George’s mjini Cape Town.

Baada ya kuagwa, mwili wa Askofu huyo ulifanyiwa utaratibu wa kuyeyushwa “Aquamation” katika hafla binafsi ya misa kama ilivyokuwa matakwa yake pindi akiwa hai.

AQUAMATION NI NINI?
Huu ni utaratibu ambao mwili huwekwa kwenye mfuko wa hariri na kisha huwekwa kwenye mashine ya Alkaline ya Hydrosis ambapo kimsingi ni bomba la chuma lenye mchanganyiko wa presha ya juu ya maji na hidroksidi ya potasium yenye kuchemshwa kwa joto hadi la 150 nyuzi Centigredi kwa saa moja na nusu.

Tishu za mwili hupasuka katika mchakato huo na mifupa tu inabaki, baada ya hapo mifupa hiyo huoshwa kwa joto la 120 nyuzi Centigredi, kukaushwa na kusagwa kwa unga kwa kutumia mashine iitwayo kremulator.

Majivu hukabidhiwa kwa familia na yanaweza kuwekwa, kuzikwa au kutawanywa kulingana na matakwa ya marehemu

Pumzika kwa Amani mtu wa watu Desmond Tutu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad