Nani anasema Mukoko ataondoka- CEO wa Yanga Senzo Mbatha



CEO wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha ameshangazwa na tetesi zinazodai kuwa kiungo wao raia wa Kongo, Mukoko Tonombe anaondoka ndani ya timu.

‘‘Nani anasema Mukoko ataondoka, ni tetesi tu zinazotokana na hali ya kwamba Mchezaji wetu sasa hapati nafasi kama ilivyokuwa wakati uliopita, lakini nampongeza sana Mukoko kwa kuwa professional.
Unapoona timu ina ushindani mkubwa wa namba, then unajua una muelekeo mzuri.’’ – Senzo Mbatha

Senzo ametoa kauli hiyo hii leo Januari 3, 2022 kupitia kipindi cha SportsBar kinachorushwa na Clouds Media.

Kumekuwa na tetesi kuwa nyota huyo, Mukoko anatimka ndani Yanga na kujiunga na watani wao wa jadi Simba SC.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad