Nani kuchukua nafasi ya Naibu spika

 


Kuteuliwa kwa Dk Tulia Ackson kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania uspika wa Bunge la Tanzania kunahamishia vita kwenye nafasi ya unaibu Spika.


Kutokana na wingi wa wabunge wa CCM ndani ya Bunge la 12, linamhakikishia Dkt. Tulia kutokuwa na kipingamizi cha kuukwaa uspika na kuacha vumbi kuanza kutimka kumtafuta mrithi wake ili kujaza nafasi.


Akizungumza jijini Dodoma jana baada ya kupitisha jina la Dk Tulia, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alisema jina la atakayegombea nafasi ya Naibu Spika litatajwa baadaye.


Ibara za 85 na 86 za Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 zimezungumzia uchaguzi wa Naibu Spika na kufafanua mazingira ambayo yakitokea basi uchaguzi wa Naibu Spika unaweza kufanyika kwa kupiga kura ya siri.


Ibara ya 85.1 ya Katiba inasema “Kutakuwa na Naibu wa Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na wajumbe kutoka miongoni mwa Wabunge.”


Ibara ya 86 inasema uchaguzi wa Naibu wa Spika, utafanywa kwa kura ya siri na utaendeshwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad