Nukuu za Rais Samia baada ya kutunukiwa vazi mkoani Kilimanjaro ‘Mimi ni Chui Jike’



Ni January 22, 2022 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan ameshiriki Tamasha la Utamaduni Mkoani Kilimanjaro.

Katika hafla hiyo Mheshimiwa Rais alikabidhiwa vazi na kupewa nafasi ya kuzungumza mbele ya waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
“Nimefurahi kuja hapa nimetunukiwa vazi hili, hapa waimbaji walisema Mimi ni Simba jike lakini kwa vazi hili mimi ni Chui Jike, kwahiyo nashukuru kwa vazi hili la kimila lakini inanipa faraja kuwa kuna Chui Dume Chifu Mariale na yeye amevaa vazi kama hili”- akiongea Rais Samia Suluhu Hassan katika tamasha la Utamaduni
“Kumekuwa na maneno mengi ndani ya Tanzania kuhusu Serikali kushirikiana na Uchifu nataka niseme kwamba tumeamua kuwa na Jukwaa la pamoja baina ya Serikali, Machifu na Wazee wa Kimila ili tushirikiane kuhifadhi mila na desturi zetu”- Rais Samia

“Tutaendelea kuimarisha bajeti ya Wizara ya Utamaduni ili iweze kuwa na uwezo zaidi wa kushirikiana na machifu katika kuzibaini kuzitangaza Mila na Desturi zetu“- akiongea Rais Samia Suluhu Hassan katika tamasha la Utamaduni

“Katika kikao cha Dodoma kati ya Machifu na Wizara ya Utamaduni ilikubalika kuwepo kwa Jukwaa la pamoka baina ya Serikali na Machifu la kila Mwaka ambalo hoja na masuala ya Machifu yatajadiliwa na kutolewa ufafanuzi au kutatuliwa nataka niwape taarifa Machifu wenzangu kwamba jukwaa hili nitaliongoza Mimi mwenyewe”- akiongea Rais Samia Suluhu Hassan katika tamasha la Utamaduni
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad