Olamide Afanikiwa Kumfikisha Fire Boy Kileleni, Wabongo Tunakwama Wapi


@fireboydml alianza harakati za muziki akiwa chuo kikuu, then akapata bahati ya kufahamiana na Olamide, @olamide baada ya kupenda uimbaji wa kipekee na aina ya kipekee ya muziki wa Fireboy akaamua amsign katika LABEL yake "YBNL" mwaka 2018. Mwishoni mwa mwaka 2018 Fireboy akaachia wimbo wake wa qkwanza "JEALOUS" (Track namba 4 katika Album yake ya kwanza)

Mwanzoni mwa Mwaka 2019, Fireboy chini ya YBNL akaachia album yake ya kwanza, "LAUGHTER, TEARS AND GOOSEBUMPS". Album hii inangoma 13 (Vibration, Jealous, Energy, scatter, King n.k) wala hakumshirikisha msanii yoyote yule katika album hii. Ngoma zote aliimba yeye na cha ajabu zaidi kumbe Album hii nzima ilitengezezwa ndani ya siku tano tu.

Album hii ilileta mafanikio makubwa sana maana alijulikana Africa nzima ndani ya muda mfupi sana, ngoma ya "Jealous", "Vibration" zilifanya vizuri sana ndani naa nje ya Nigeria.

Ni Bandika Bandua, mwaka 2020 akachia album ya Pili "APOLLO" album hii inanyimbo 17 na alishirikisha baadhi ya wasanii-Wande Coal, Olamide na D Smoke. Album hii pia ilifanya vizuri sana, ngoma kama Champion ilikuwa Kubwa sana.

Mwaka 2021, Fireboy ametoa single kadhaa, na moja wapo ni PERU, single hii imepelekea Remix kubwa sana, Fireboy Featuring Ed Sheeran, imagine ukubwa wa Ed Sheeran lakini ameielewa Ngoma na amekubali kuingia studio na kufanya remix.

Mbali ya Fireboy kufanya kazi na Ed Sheeran, hivi sasa kuna clip inamuonesha Chris Brown akicheza ngoma hiyo "PERU", haya ni mafanikio makubwa sana, Fireboy anapita njia Za Wizkid.

All in all, Olamide anamchango mkubwa sana katika Mafanikio ya Fireboy kwasababu yeye ndio kamtambulisha katika Muziki na ni ndani ya miaka mitatu tu Fireboy kawa wa kimataifa akiwa chini ya YBNL.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad