Ombi la Sabaya Lakubaliwa Mahakamani




MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha imekubali ombi la mawakili upande wa utetezi kuondoa ushahidi wa picha za CCTV zilizokuwa ziwasilishwe na Afisa Uchunguzi wa Takukuru, Ramadhan Juma katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Juma ambeye ni Shahidi wa 13 alipaswa kutoa ushahidi wa kiuchambuzi wa picha za video zilizo rekodiwa tarehe 22 Januari, 2021, hata hivyo mawakili wa utetezi walipinga kwa kuwa shahidi huyo hana mamlaka kisheria.

Hakimu Patricia Kisinda aliiambia Mahakama Jumatatu kuwa imeridhia hoja za mawakili wa upande wa utetezi kutokana na Sheria ya Ushahidi no 17 na kwa kurejea Maamuzi ya Mahakama za juu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad