Ameandika msanii wa muziki wa kizazi kipya @ommydimpoz
"Bismillaah: Yapo Mengi Ya Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Mwaka Uliopita Yapo Malengo Yaliyofanikiwa na ipo mitihani Ambayo pengine imeleta kikwazo kwenye Malengo yetu.
"Jambo la Muhimu ni Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Afya na Uzima na kuwaombea wale Walio kitandani Waweze kuinuka. Kitu nilichojifunza na Nachoendelea kujifunza kwa Walionizidi iwe kiakili ama ki Fedha ni kuwa kila jambo linawezekana.
"Cha muhimu ni kupambania ndoto zetu na kuwa focused Hakuna aliyesomea Maisha, Ukiwa na Nidhamu na Juhudi huku ukimuomba Mungu basi jua Wakati wako utafika na Riziki yako itaongezeka wala tusioneane Choyo.
"Pale Mwenzako anapopiga hatua, tusikate tamaa wala kuhuzunika pale unapopata vikwazo kwenye utafutaji wetu kwani hata mitume ilipigwa vita na kuchukiwa itakuwa wewe mtoto wa Binti Saidi 😃."
HAPPY NEW YEAR 2022"