Hivi karibuni matandao wa Webometric ulitoa viwango vya ubora wa vyo vikuu duniani, chapisho ambalo lilihusisha vyuo vikuu 5,000 kutoka mataifa mbalimbali.
Viwango hivyo vya ubora vilizingatia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuangalia tovuti za vyuo husika kama zina taarifa muhimu pamoja na machapisho ya tafiti, machapisho ya kitaaluma, kazi za kibunifu na taarifa nyinginezo za kitaluuma kwa ngazi ya kimataifa.
Katika orodha hiyo, vyuo vikuu vya Tanzania havijafanya vizuri, kwani chuo cha kwanza kilichopo katika nafasi ya juu zaidi ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambacho kimeshika nafasi ya 1913 duniani, huku kikwa cha 42 kwa ubora Afrika.
Hapa chini ni orodha ya vyuo vikuu 10 bora zaidi Tanzania kwa mujibu wa mtandao huo. Namba ya mbele ni nafasi ya chuo hicho Afrika:
1. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)- 42
2. Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)- 51
3. Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)- 91
4. Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)- 174
5. Chuo Kikuu Mzumbe- 203
6. Chuo Kikuuu cha Kanisa Katoliki cha Sayansi za Afya (CUHAS)- 219
6. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT)- 249
7. Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)- 256
8. Chuo Kikuu Ardhi- 265
9. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM -AIST)- 280
10. Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (TUMa)- 286
Baadhi ya wadau waliotoa maoni yao kuhusu orodha hiyo, mathalani vyuo vya Tanzania kutokufanya vizuri wamesema kuwa ifahamike kwamba Webometric wao hawaangalia kigezo cha ubora wa taaluma, bali wanaangalia tovuti za vyuo husika kuona kama zina taarifa na machapisho mbalimbali, kuona kama wahadhiri wanashirikiana na wenzao wa kimataifa.
Wadau hao wamehimiza vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuweka uwazi katika utendaji kazi kimataifa na kuviwezesha vyuo na taasisi hizo kushika nafasi za juu.