Pablo akunwa na kiwango Simba



KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amesema amefurahishwa kuona mpira wa kuvutia kutoka kwa vijana wake kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Namungo FC.

Simba iliibuka na ushindi wa 2-0 kwenye mchezo huo na itacheza na Azam FC, kwenye fainali itakayopigwa kesho Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Pablo alisema mchezo dhidi ya Namungo ulikuwa wa kiufundi na kimbinu ulikuwa mzuri na wachezaji wake wamepambana na kupata matokeo mazuri.

Alisema wanasahau matokeo hayo na wanaenda kujipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao wa fainali na kutwaa ubingwa wa Mapinduzi.

“Azam FC ni timu nzuri na ana imani utakuwa wa ushindani mkubwa, kutokana na ubora wa wapinzani wetu tunaenda kujiimarisha zaidi ili kufikia malengo,” alisema Pablo.


 
Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, alisema malengo yao ni kutafuta ushindi katika kila mechi na sasa wanajipanga kwa mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC.

Alisema wachezaji wamekituma na kufanikiwa kutinga nusu fainali dhidi ya Namungo FC na  kucheza mpira biriani ambao waliukosa kwa muda mrefu.

“Wachezaji wamecheza ule mpira ambao tuliukosa muda na sasa umerudi, tumeweka mikakati ya kuhakikisha tunaenda kupambana na kutwaa ubingwa wa Mapinduzi,” alisema Barbara.


Alisema kuhusu usajili wataweka wazi siku ya mwisho ya kufunga dirisha la usajili kwa kuweka wazi majina ya wachezaji waliowasajili kuongeza nguvu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad