Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Franco Pablo Martin amesema anajihisi vibaya kuona baadhi ya wachezaji wake wakishindwa kuitumia vyema mipira iliyokufa (Penati), ili kuipatia mabao timu hiyo.
Simba SC msimu huu imeshapoteza Penati zaidi ya tatu katika Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kimataifa, jambo ambalo limeibua sintofahamu kwa Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo.
Akizungumza na Wanahabari kisiwani Unguja-Zanzibar Kocha Pablo amesema kama Kocha hajihisi vizuri kuona tatizo hilo likiendelea, hivyo amedhamiria kulitatua na kulimaliza kabisa.
Dili la Chiko Ushindi lazimwa Young Africans
“Sifuraishwi na namna wachezaji wangu wanavyoshindwa kutumia vizuri mipira iliyokufa hususan Penati, haileti taswira nzuri kwa timu nitalifanyia kazi hilo.” amesema Kocha Pablo
Wachezaji waliokosa Penati Simba SC msimu huu ni Nahodha na Mshambuliaji John Bocco dhidi ya Biashara United Mara, Erasto Nyoni dhidi ya Ruvu Shooting, Rally Bwalya dhidi ya Azam FC huku Bernard Morisson akikosa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Red Arrows ya Zambia.
Pablo: Nimeshakabidhi ripoti
Simba SC ipo Zanzibar kwa ajili ya Michuano ya Mapinduzi, na leo Jumatano (Januari 05) itacheza dhidi ya Selem View Uwanja wa Aman kuanzia saa Kumi Jioni.