Mwanamke mmoja kutoka mji wa California nchini Marekani, Fatima Madrigal amejifungua watoto mapacha wawili waliopishana dakika 15, mmoja akizaliwa mwaka 2021 na mwingine mwaka 2022.
Fatima na mumewe Robert Trujillo walipata watoto hao ambapo mmoja wa kiume alizaliwa Desemba 31 majira ya saa 5:45 usiku aliyepewa jina la Alfredo na baada ya dakika 15 ambayo ilikuwa ni saa 6 usiku na siku nyingine mpya na mwaka mpya wa 2022 walipata mtoto mwingine wa kike aliyepewa jina la Aylin.
“Kwangu ni ajabu kuwa hawa ni mapacha lakini si was siku wala mwaka mmoja,” alisema Fatima katika taarifa iliyotolewa na hospitali alipojifungulia.