Panya Magawa wa Tanzania, shujaa wa kutegua mabomu afariki Dunia Cambodia



Panya shujaa wa Tanzania aliyetumika kutafuta na kutegua mabomu ya ardhini  na vilipuzi -Magawa amefariki dunia mwishoni mwa wiki .


Kupitia taarifa katika ukurasa wake wa instagran ,shirika la Apopo limesema Magawa alikuwa na afya njema wiki jana lakini afya yake ilianza kudhoofika mwishoni mwa wiki na kuaga dunia akiwa na umri wa miaka minane .

Panya huyo alisifika sana kwa kusaidia kugunduliwa kwa Zaidi ya mabomu 100 ya kutegwa ardhini nchini Cambodia .

‘Mchango wake unaruhusu jamii nchini Cambodia kuishi, kufanya kazi na kucheza; bila hofu ya kupoteza maisha au kiungo.


 
Mnamo Septemba 2020, alikabidhiwa rasmi Medali ya Dhahabu ya PDSA – tuzo ya juu zaidi ya ushujaa ambayo mnyama anaweza kupokea. Mwaka jana wakati Magawa alipostaafu, HeroRAT Ronin alichukua kijiti kama panya mpya wa kuasili.’ Imesema sehemu ya taarifa iliyotangaza kifo cha panya huyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad