Basi humu duniani hakuishi vituko kila kuchao. Mchungaji mmoja raia wa Ghana, amezua mjadala moto mtandaoni kwa kupeperusha video mubashara ya mkesha wa Mwaka Mpya akiwafanyia washirika wa kike tambiko ya kushangaza.
Katika video inayosambaa kama moto mtandaoni, pasta huyo anasikika akiwambia kondoo wake wajitokeze haraka kwa "kuoga takatifu"
Baadhi ya washirika wanaonekana wakivua nguo zote na kubaki uchi wakiingia ndani ya beseni na baada ya kuogeshwa, pasta mwingine anaonyeshwa akiwapaka mafuta takatifu.
Pasta huyo pia anasikika akisema kuwa licha ya kufahamu kwamba hatua hiyo itazua utata, hana budi ila kuheshimu maagizo ya roho mtakatifu.
Huku mtumishi huyo akiwaogesha kondoo wake wa kike, mwingine nchini Nigeria amezindua chupi na sindiria zenye chapa ya picha yake ili kuwasaidia wanawake waseja wanaotamani kuolewa kuwavizia waume zao.
Kulingana na pasta Dr J.S. Yusuf, ambaye ni mkuu wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International mjini Abuja, aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za 'baraka' ili kufungua milango ya ndoa Mwaka Mpya.
Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema “Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.”
Pia alisema kuwa chupi hizo zinapovaliwa na wanawake, zitawasaidia kupigana na magonjwa na kupata bahati njema ya kuwavizia wanaume ambao watawaoa.
Itakumbukwa kwamba si mara ya kwanza kwa watumishi wa Mungu kufanya mambo ya kiajabu hususan wanaotokea katika mataifa ya magharibi mwa Afrika.
Mhubiri ambaye ni raia wa Ghana, Osofo Acheampong, alitoa kauli nzito kwa kusema kwamba sio vibaya kwa mwanamume kuwa na mpango wa kando hata ingawa ni mume wa mtu.
Zawadi ya Krismasi: Mama Gatundu Ajifungua Watoto Watatu Mkesha wa Krismasi
Pasta Acheampong, anayesemekana kuwa kiongozi wa Kanisa la Kipentekosti la Sabato, alitoa maoni hayo kwenye mahojiano ya hivi punde huku akitoa mafungu ya Bibilia kuipa uzito kauli yake.