Pigo kwa taaluma ya Kiswahili mtaalam akifariki




TAALUMA ya Kiswahili imepata pigo kufuatia kifo cha mtaalamu wa Kiswahili, Sheikh Abdilahi Nassir, siku ya Jumanne nyumbani kwake, Mombasa.

Sheikh Nassir aliandika Kamusi ya Shule za Msingi (Oxford University Press, 2007) kwa ushirikiano na Maprofesa John Gongwe Kiango, Abdulziz Y. Lodi na Isaac Ipara Odeo.

Akizungumza na Taifa Leo kwa njia ya simu, Prof Abdulaziz Y. Lodhi anayefundisha katika Chuo Kikuu cha Uppsala, nchini Uswidi alisema, “Marehemu Nassir alishiriki kikamilifu katika siasa za Kenya kuanzia 1957 – 1963, kisha akateuliwa kuwakilisha Kenya katika Baraza la Bunge kabla ya Uhuru (Legislative Council) kati ya 1961- hadi 1963.”

“Akiwa mwanachama wa Legislative Council, marehemu pia alihudhuria kongamano la kihistoria kuhusu Katiba ya Kenya, lililofanyika katika Bunge la Lancaster, jijini London, Uingereza mnamo 1963,” akasema Prof Lodhi.


 
Alikuwa kaka yake mshairi na mwanaharakati maarufu Abdilatif Abdalla anayefahamika kwa diwani yake ya mashairi Sauti ya Dhiki (Oxford University Press, 1973).

Mbali na uanaharakati, marehemu Sheikh Adbilahi Nassir, aliwahi kuwa mhariri wa Kiswahili katika mashirika ya uchapishaji kama vile Oxford University Press na Shungwaya Publishers mnamo miaka ya 1970.

Kabla ya mauko yake, marehemu alikuwa anajishughulisha na anatafsiri na kuandika tahakiki ya Kiswahili kuhusu Kurani Tukufu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad