Meneja wa Habari na Mawasilino wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally amehoji tukio la Kiongozi wa Young Africans kuingia Uwanjani dakika chache kabla ya kuanza kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ uliochezwa Jumamosi (Januari 29), Uwanja wa CCM Kirumba.
Young Africans walikua wenyeji wa Mchezo huo uliohamishwa kutoka Dar es salaam na kupelekwa Mwanza, ambapo kabla ya kuanza, nahodha wa kikosi cha ‘Wananchi’ Bakari Nondo Mwamnyeto alimkabidhi jezi Hersi Said kama ishara ya kumpongeza kwa kupata mtoto wa kiume.
Ahmed Ally amehoji tukio hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika: Kwa mujibu wa kanuni ya 17 ya Ligi hairuhusiwi mtu asiyehusika na mchezo kuingia Uwanjani wakati mchezo unaendelea.
Huyu Kiongozi anaingiaje kwenye pitch wakati mchezo umeanza tena kwa tukio lisilokua la kimichezo?
Anapataje ruhusa ya kuingia Uwanjani kupongezwa juu ya uzao wa Mtoto tena Kick Off inasimamishwa Ili wao wapongezane.
Mmewahi kuona wapi hili likitokea?
Tukio halijaja bahati mbaya, kawaida lazima utoe taarifa kwa Kamishna wa mchezo juu ya kufanyika kwa tukio kama hilo?
Kamishna alikubali kwa vigezo vipi tukio lisilokua la kimichezo lifanyike kwenye mechi rasmi ya kimashindano?
Na kama hawakuomba ruhusa huyu anatoa wapi mandate ya kufanya hivyo??
Huku ni kuunajisi mpira, ipo siku mtu atataka kumvisha Pete mchumba ake halafu atafanya hivyo kwenye mechi
TFF tafadhalini simamiemi misingi ya mpira.
Udhamini wa Bilioni 1 kwa Mwaka usiwatie upofu.
Nasema haya sio kwa sababu ya upinzani ni bali tunataka taratibu za mpira zifuatwe ili tuwe na mashindano bora zaidi.