Rais wa Kazakhstan, Kassym-Jomart Tokayev amewaamuru Jeshi la Polisi na Wanajeshi wa nchi hiyo “kuua watu bila onyo” ili kukomesha maandamano ya vurugu ambayo yamelemaza Jamhuri ya zamani ya Usovieti na kuripotiwa kusababisha vifo vya makumi ya watu.
Katika hotuba yake kwa Taifa jana Ijumaa, Tokayev alidai machafuko hayo yaliyoanza wiki hii kama maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta, yalipangwa na “majambazi wa kigaidi” waliopewa mafunzo kutoka ndani na nje ya Nchi hiyo na tayari Askari 18 na “wahalifu wenye silaha” 26 wameuawa katika maandamano hayo yenye vurugu.
Kwenye Jiji la Almaty ambalo ni kubwa zaidi nchini humo, maiti kadhaa zilizokuwa zimejaa risasi zilionekana zimeachwa barabarani ambapo baadhi ya huduma muhumu zimekatika pia ikiwemo kukatika kwa mtandao kwenye mashine za ATM.