“Niliingia kwenye siasa kwa kuwa nilikuwa nina sababu moja tu.
“Nilipokuwa naangalia mijadala ya Baraza la Wawakilishi nilikuwa naona kuna vitu haviko sawa, nilitaka niingie niisimamie serikali, niwapambanie wananchi kwa kuwa nimefanya nao kazi muda mrefu kwa muda wote niliokuwa NGO.
“Nilikuwa nikiona kuna mawaziri wanajibu tofauti kile kilichopo kwa wananchi.
“Sikujua mtu anaingiaje huko, nikauliza, nikanifahamisha, nikaamua kurudi mkoa wangu nilikozaliwa Kusini Unguja.
“Wengi walikuwa wakinifahamu kwa jina la Bibi Mchele, kwa kuwa niliwahi kuwasaidia kupitia World Food Program kulipotokea matatizo ya wadudu kuvamia mazao.
“Tuligawa mafuta, mchele, samaki…ndiyo maana nilipoenda wakasema ‘Ahh kumbe ni Bibi Mchele, tunampa’, ndipo nikapita kupitia viti maalum,” - Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika siku yake ya kuzaliwa, leo Ikulu, Januari 27.