Rais Samia Atoa Maagizo kwa RC Makalla

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali iko mbioni kuanza ujenzi wa soko jipya eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam ikiwa sehemu ya mkakati wa kuwa na masoko katikati ya mji yatakayofanya kazi saa 24.


Rais Samia amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amosi Makalla kuanza utaratibu wa manunuzi na kumtafuta mkandarasi atakayejenga soko hilo.


Ameyasema hayo leo Jumanne Januari 25, 2022 alipokuwa akizungumza na viongozi wa wamachinga Ikulu, Dar es Salaam, wiki moja baada ya soko la Karume kuungua na kusababisha hasara ya Sh7.2 bilioni.


Rais Samia ameeleza kuwa “Moto huu una sababu kadhaa, Kariakoo tuliambiwa hitilafu ya umeme, Karume ripoti ya awali tunaambiwa mishumaa lakini hata moto unapoendelea magari yakiwa yanakuja hayana maeneo ya kupita na kwenda kuzima moto, tujipange ili magari yaweze kupita kwa urahisi, wale wanaopika kuna ile ‘nabandika maharage kesho nikija nitakuta yameiva’ inawezekana kabisa moto ukashika kitu moto ukaendelea”.


“Lingine ni suala la Bima kuna wale ambao labda amekata Bima ya biashara yake lakini kwa miaka kadhaa hajafaidi matunda ya Bima yake kwahiyo anaamua tu ‘ngoja niweke kicheche cha moto hapa kukiungua Mimi kwasabau nina Bima nitalipwa na Bima’ hilo nalo lipo”.


“Jingine ni hawa wanaochukua mizigo madukani inawezekana Mtu kachukua mzigo mkubwa kauza, moyo wa ushetani unamtuma asiende kurudisha, weka moto mwenye duka atajua soko limeungua au karume imeungua kwahiyo sina cha kulipa na huenda mwenye duka ana bima atalipwa huko, ndio maana nimesema tumekua sasa tujisimamie,” amesema Rais Samia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad