Rais Samia: Kama humpendi Samia mheshimu Mungu aliyempa urais



RAIS Samia Suluhu Hassan amesema wafunda na kuwaonya mawaziri kutambua kuwa urais ni taasisi na sio mtu, hivyo kama hawampendi Samia aliyepo madarakani basi wamuheshimu Mungu wao kwa kujua kwamba amewekwa na Mungu huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu (endelea)

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Januari 2022 jijini Dodoma wakati akizungumza katika mkutano maalumu wa mawaziri na manaibu wote waliopo katika Baraza lake la Mawaziri.

Amesema urais ni taasisi kwa sababu mtu anawekwa kufuata Katiba na mambo mengine ndio maana kati yao mmoja lazima awe rais.

Amesisitiza urais ni taasisi ambayo inakuja na mamlaka yake, inatoa miongozo hivyo yeyote anayekuwepo ndani ya Baraza la Mawaziri na Serikali anafanyia kazi taasisi ya urais na kama humpendi rais aliyepo anatakiwa kuipenda nchi.


 
“Tunaambiwa kwamba mamlaka na uongozi wowote unatoka kwa Mungu, si ndio? Na sisi sote hapa tuna dini zetu na tunaamini Mungu, si ndio? Sasa kama humpendi aliyepo muheshimu Mungu wako kwa kujua kwamba aliyepo amewekwa na Mungu… muheshimu tu Mungu wako.

“Samia aliyepo, Samia simpendi! usimpende tu… kwa hiyo sio usimpende yeye ukapuuza na yote yanayozunguka hiyo taasisi aliyopo, hapana! Yale yanayotokana na taasisi yaheshimu, mchukie yeye tu!

Pamoja na mambo mengine amewaeleza mawaziri hao wakiongozi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa mzigo walioubeba na kiapo walichoapa ni kikubwa.


“Lakini tuliapa kiapo cha maadili ambapo ndani yake kuna mambo mengi mmeyasema kwa midomo yenu, sitotumia nafasi yangu kwa ajili hii… lakini tukifutilia mmoja mmoja wengi wetu kile kiapo hatukifuati.

“Nina mafaili ya assessment ya kila mmoja wenu rundo. Wote tuna kasoro zetu, lakini zile kasoro zisizidi yale tunayofanyia kazi. Duniani hakuna mtu ambaye mkamilifu kwa asilimia 100, wote tuna kasoro zetu lakini zile kasoro zisizidi tunayofanyia kazi,” amesema Rais Samia.

Aidha, pamoja na hilo Rais Samia amewafunda mawaziri hayo kuhusu mambo mbalimbali tisa ikiwa kutunza siri zetu za serikali, kujenga utamaduni wa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa kazi mbalimbali za serikali na kutatua kero za wananchi na ufuatiliaji wa karibu wa miradi ya Taifa.

Mengine aliyowaonya ni kutoelewana baina yao, kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na ushauri wa watalaam katika utendaji wa kazi, kuwa wabunifu na kutatua changamoto na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea, kufuata taratibu zote katika kuhakikisha watumishi wasiowajibika, wanatimiza tu wajibu na mwisho kutambua kuwa duniani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad