“Mafaili ni mengi, najitahidi yasilale kwangu yaende kwa wenzangu, wakati mwingine kulala saa saba usiku.
“Nikilala na faili juu ya meza ujue siku hiyo nimechoka sana, ukiacha mafaili kazi ni nyingi pia.
“Ukijua kuwatumia wasaidizi, hauwi mzigo mkubwa sana, kwa kuwa unaurudisha kwao ili nao wafanye, ndiyo maana katika vikao vingi na wasaidizi wangu nawasisitiza wafanye maamuzi,” - Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika siku yake ya kuzaliwa, leo Ikulu, Januari 27.