Refa Aliyevurunda Mechi ya AFCON Jana Alikuwa Mgonjwa



Mkuu wa waamuzi wa #AFCON2021 Essam Abdel-Fatah amefichua kuwa Janny Sikazwe alijihisi vibaya kiafya (KIHARUSI CHA JOTO) wakati wa mchezo wa Tunisia na Mali na kusababisha kupoteza umakini.

Kiharusi cha joto ni hali inayosababishwa na joto la juu la mwili wa binadamu. Refa huyo katika dakika ya 79:43 alimwambia mwamuzi wa akiba aongeze dakika 5,akimaanisha kuwa 90 zimekamilika kumbe bado.

Cha ajabu ilipofika dakika ya 85 akapuliza kipyenga kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo na kusababisha mabishano kabla ya kuanzisha upya mchezo huo na kisha kupuliza kipyenga cha kuumaliza tena mchezo huo dakika ya 89.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad