Rick Ross Ajikomba Upya Kwa Hamisa



BAADA ya kumchunia na kusababisha mwanamama Hamisa Mobeto  kusemwa kuwa ametoswa na rapa wa Marekani, Rick Ross, hatimaye jamaa huyo ameanza tena kujikomba kwa mwanamitindo huyo.

 

Tangu mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, Rick Ross ambaye baadhi ya Wabongo wanamuita Mpoki alikuwa kimya, lakini wikiendi iliyopita amerejea na kuanza kumsifia upya Hamisa baada ya kuona video yake inayomuonesha akinyonga mauno kiufundi.

 

Baada ya Hamisa kuposti video hiyo ndipo Rick Ross akaibuka na kuweka emoji za motomoto kama zote, jambo linalotafsiriwa kwamba jamaa amerejesha majeshi.

 

Mwaka jana, Hamisa na Rick Ross walikutana Dubai na kula bata kama lote ambapo baadhi ya mashabiki wamwanamitindo huyo wa kimataifa za Tanzania waliamini wangeenda mbali zaidi na kuwa mke na mume.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad