Rubani wa Ndege ndogo iliyopata ajali na kunasa kwenye njia ya Treni amenusurika kifo baada ya kuokolewa


Rubani wa Ndege ndogo iliyopata ajali na kunasa kwenye njia ya Treni amenusurika kifo baada ya kuokolewa na Polisi wa Los Angeles, Marekani sekunde chache kabla ya treni ya kasi kupita na kuigonga Ndege hiyo na kuipasua vipandevipande.

Video iliyotolewa na Polisi wa Los Angeles ikiwa imrekodiwa kutoka kwenye camera ambazo huvaliwa na Polisi imeonesha jinsi Polisi walivyomvuta Rubani huyo kutoka kwenye Ndege akiwa anatokwa damu kutokana na majeraha ambapo sekunde chache baadae ilipita treni kwa spidi na kuisambaratisha Ndege hiyo.

Rubani huyo alikuwa peke yake kwenye ndege hiyo ambapo aliwaishwa Hospitali kwa ajili ya matibabu baada ya kuokolewa na Polisi hao wanne.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad