Moja kati ya vitu ambavyo mwanamuziki #ruby amevitolea majibu ni pamoja na swali kuhusu kitu gani kiliwahi kumkera kwenye mahusiano yake yaliyopita.
Sasa #Ruby kupitia insta story yake akijibu moja kati ya maswali kutoka kwa mashabiki zake amefunguka kuwa moja kati ya kitu kimewahi kumkera kwenye mahusiano yake yaliyopita na mwanamuziki mwenzake @kusah ni swala la Uchawi / imani za Kishirikina kutoka kwa aliyekua mpenzi wake huyo ambae amefanikiwa kuzaa nae mtoto mmoja wa kike.
Hata hivyo #Ruby hakufafanua zaidi kuhusu madai hayo, zaidi ya kujibu tu kwa ufupi katika kile alichodai kuwa anajiskia kuwa mkweli.