Samia: Acheni Kuwachafua, Lukuvi na Kabudi Nina Kazi Nao



Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watu kupuuza maneno maneno yanayoendelea na kwamba aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi atampa kazi maalum ambayo ataitangaza hivi karibuni huku akabainisha kuwa Lukuvi hatogombea nafasi ya Spika wa Bunge.


Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu, Januari 10, 2022 Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma wakati akiwaapisha mawaziri, manaibu waziri na makatibu wakuu aliowateua hivi karibuni.


“Kaka zangu hawa (Profesa Kabudi na William Lukuvi) bado nina kazi nao, nimewavuta Ikulu. Acheni maneno maneno wamefanya kazi nzuri, na wamelitumikia Taifa kwa uadilifu na uaminifu mkubwa, waacheni waje kwangu tumalize nao pamoja.


“Nimeona meseji nyingi nyingi, afadhali Lukuvi katoka, hajatoka yupo, wengine wameanza kumletea meseji wakijua atagombania Uspika, hatagombania, msianze kumchafua, ametumikia Taifa hili kwa uadilifu.

“Nina kaka zangu wawili William Lukuvi na Profesa Kabudi, wana umri kama wangu, na ukiwatazama niliowateua hamfanani kabisa, kwahiyo kaka zangu wawili hawa nimewavuta kuja kwangu Ikulu ili waje wanisimamie kuwasimamia nyie.


“Kaka yangu Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia mazungumzo ya serikali na mashirika na ndiyo kazi ambayo sasa nataka nimkabidhi kindakindaki, aendelee na kazi hiyo, yeye ni Baba mikataba.  Lukuvi ana kazi maalum na mtaisikia hivi karibuni,” amesema Rais Samia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad