“Wakati moto unaanza nilikuwepo mimi ni moja ya Walinzi wa siku hiyo, sikuwa mbali na banda lililoanza kuungua niliitwa na kwenda kuanza kupambana kuzima moto, ilibidi tukate bomba la choo cha Halmashauri na kuchukua ndoo za choo hicho ili kuweza kuuzima moto japo ulituzidi nguvu"
"Chanzo cha moto ni Mateja ambao tupo nao sokoni Karume, wao wanajihusisha na kuuza viatu, pale sokoni kuna moja ya banda ambalo wao wanalitumia kutengeneza mihadarati yao ambayo huwa wanatumia mishumaa kuitengeneza, siku hiyo mshumaa ulianguka na kuanza kuungua”
——— Thomas Benedicto, Mfanyabiashara na Shuhuda wa moto wa Soko la Karume akizungumza kwenye Power Breakfast ya @CloudsFMTZ