Simba Wakamilisha Mchongo wa Usajili...Chama Awa Gumzo Mwenyekiti wa Usajili Afunguka


Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Kassim Dewji amesema klabu hiyo imefunga usajili wao msimu huu. Amesema watamtambulisha nyota mpya kutoka nje ya nchi ambaye ndiye amewafungia usajili wao wakati huu wa dirisha dogo.

“Tayari tumekwishamaliza naye, ila sitomtaja jina na nchi anayotoka sababu utamfahamu, lakini tumemalizana naye na hivi karibuni atatambulishwa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, Try Again (Salim Abdallah)” amesema Dewji.

Hivi karibuni Simba kwenye mkutano mkuu ilifichua kuwa na mpango wa kumrejesha Cleotus Chama. Katika hotuba yake, Try Again alisema watamrejesha mchezaji huyo jambo ambalo lilishangiliwa na mamia ya wanachama wa klabu hiyo waliojitokeza kwenye mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam.

Kuhusu wachezaji waliokuja nchini kwa ajili ya majaribio kwenye timu hiyo, Kassim Dewji amesema hakuna hata mmoja atakayesajiliwa na klabu hiyo msimu huu.

“Mawakala wao ndiyo waliomba waje kufanya majaribio, kama klabu hatukuona sababu ya kuwakatalia, lakini kama nilivyosema hakuna hata mmoja ambaye atasajiliwa kati yao kwenye timu yetu” amesema.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad