↪️ Taarifa kutoka kwa vyanzo vyangu ni kuwa tayari Msuva alipeleka madai yake FIFA tangu December, 2021 kuhusu malipo ya signing dhidi ya Wydad Casablanca
↪️FIFA wamepokea madai hayo ila huchukua muda kuanzia miezi mitatu mpaka sita Ili kutuma taarifa kwa Klabu husika (Wydad) waanze kutoa utetezi wao
↪️Baada ya huo utetezi ndipo FIFA watakaa chini kupitia wanasheria wake kutazama upande wa Msuva na wa klabu kuhusu hayo madai yake kisha kutoa maamuzi
↪️Msuva yupo Bado nchini kwasasa na FIFA huwa inapenda Wachezaji waendelee kucheza hata kama Wana kesi ili kulinda viwango, Msuva ni mnufaika anaweza kusaini popote akitaka
↪️Ikitokea amesaini au ameshasaini basi FIFA watatuma ITC Ili kumruhusu Mchezaji aendelee kucheza mpira popote anapotaka, mpaka kesi yake itapopata majawabu
By @jr_farhanjr