Spika wa Bunge, Job Ndugai anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa leo saa tano asubuhi Januari 3, 2022.
Spika huyo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuzungumza kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Spika, Bungeni Dodoma.
Bado haijawekwa wazi Ndugai anaenda kuzungumza kuhusu mada ipi kwa kuwa jina lake limekuwa gumzo siku za hivi karibuni hasa kutokana na kauli yake kuhusu mikopo ya nchi.