Tanesco Yatangaza Mgawo wa Umeme

 


Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kutokana na maboresho ya vituo vya kuzalisha umeme vya Kinyerezi l inayotegemewa kuzalisha megawati 185 na ubungo lll megawati 112 yatasababisha kuwepo kwa mgawo wa umeme nchini.

Hayo yamesemwa leo Januari 28, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Maharage Chande baada ya kutembelea maboresho ya upanuzi wa huduma hiyo katika mradi wa Kinyerezi l.

Amesema mpaka sasa uzalishaji kutoka mitambo ya ubungo lll umefikia megawati 60 ambazo tayari zimeunganishwa kwenye gridi ya Taifa huku kazi ya upanuzi wa kituo cha Kinyerezi l inaendelea vizuri na megawati 70 zimeanza kupatikana na ifikapo mwezi Agosti 2022 kazi hiyo itakuwa imekamilika na kupelekea kituo hicho ambacho kwa sasa kinazalisha megawati 150 kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 335.

"Mitambo hii inaongezwa ili iweze kuzalisha umeme inapelekea mahitaji ya gesi asilia kuongezeka ambapo inalazimu kufanya uboreshaji wa mfumo wa gesi kwenye mifumo ya Tanzania Petroleum Development Company,(TPDC) na Pan African Energy Tanzania,(PAET),"amesema Maharage

Amesema Shughuli ya uboreshaji litafanyika kwenye visima vya gesi vilivyopo Songosongo kuanzia februari mosi hadi 10,2022ambapo kukamilika kwake kutahakikisha gesi ziada inayotajika inapatikana .

Amesema Utekelezaji wa marekebisho hayo utapelekea mapungufu ya gesi kwenye mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi asilia na kulazimika  kuzimwa Kwa baadhi ya mitambo hiyo ili kupisha shughuli hiyo muhimu.

"Hii itasababisha upungufu wa uzalishaji umeme na kuathiri baadhi ya maeneo,na taarifa za ratiba ya upatikanaji umeme kwa Kila mkoa zitatolewa na mikoa husika Kwa wakati kwa  kipindi chote cha maboresho," amesema Maharage

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad