Tanzania Inaenda Kuwa Kama ULAYA Anwani Za Makazi Kuifanya Tanzania Ya Kidijiti

 


SERIKALI imejikita kutekeleza mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi nchi nzima kwa lengo la kuibadilisha Tanzania kuwa ya kidijitali kwa kuwa mfumo huo ni msingi wa utambuzi wa kila mwananchi.

Utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi pia utaiwezesha serikali kuwa na sensa bora

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye jana wakati akifungua mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi, watendaji na wataalamu wa Mkoa wa Morogoro kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi ambaye aliwakilishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Jim Yonazi.

Nape alisema nia ya serikali ni kuhakikisha kila mtaa, barabara inakuwa na jina la mtaa na kila nyumba inakuwa na namba. Alisema ni muhimu kukamilisha mfumo wa anwani za makazi na postikodi ifikapo Mei mwaka huu kwani jambo hilo ni la msingi na la muhimu kukamilishwa kwake kwa kipindi hicho kwani ifikapo Agosti mwaka huu kutakuwa na sensa ya watu na makazi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad