Muigizaji wa tamthilia pendwa zaidi kwa sasa ya Uturuki ya Ertugrul, bwana Ayberk Pekcan maarufu kama Artuk Bey amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 51.
Ayberk ambaye amecheza kama, Artuk Bey kwenye tamthilia hiyo ya Ertugrul, amekuwa akisumbuliwa na kansa kwa miezi kadhaa. Familia ya muigizaji huyo imethibitisha kifo chake hapo jana siku ya Jumatatu Januari 24, 2022.
Nyota huyo amekuwa kipenzi cha mamilioni ya mashabiki ambao wanafuatilia tamthilia ya Ertugrul akiwa ni miongoni mwa wahusika wakuu.
Muigizaji huyo aliwahi kuandika maelezo mafupi kuhusiana na hali yake ya kiafya miezi michache iliyopita kabla ya kifo chake
”Wapendwa marafiki…. Mchakato ambao ulianza na daktari niliyeenda kumalalamikia kuhusu maumivu ya mgongo umefikia hatua hii leo. Nina saratani ya mapafu. Pia imeenea kwenye ini na adrenal glands. Kwa bahati mbaya, ugonjwa huu haukuonyesha dalili zozote katika hatua zake za awali. Usaidizi wangu mkubwa ni pamoja na familia yangu. Vile vile na marafiki zangu walio karibu… Nitajitahidi niwezavyo kurudisha afya yangu.”
Kama kuna mwigizaji ambaye angetufundisha na sisi waTZ kucheza filamu za ukweli kuhusu enzi zetu za zamani ni huyu jamaa!
ReplyDeleteAlikuwa akinishangaza kwa namna alivyokuwa akinipeleka katika uhalisia wa Historia ya Wataki wa Uturuki niliyokuwa nimeisoma vitabuni kabla.
Mola amrehemu! Apumzike kwa Amani!