MTALII mmoja amekanyagwa hadi kuuawa na Tembo katika mbuga ya wanyama nchini Uganda, baada ya mtalii huyo kutoka kwenye gari alilokuwa akisafiria yukio hilo lilitokea Jumanne usiku.
Marehemu, ambaye ni raia wa Saudia, alikuwa akipita kwenye mbuga ya taifa ya wanyama ya Murchison Falls National Park iliyopo katika mji la Arua pamoja na wenzake wakati waliposimama kujisaidia.
Inadaiwa kuwa marehemu alitoka kujisaidia na alikwenda mbali zaidi ya gari, hakuweza kurejea.
Maafisa wa mbuga ya Wanyama walithibitisha tukio hilo na walisema upelelezi unaendelea walisema kuwa hatua zinachukuliwa kuzuwia matukio ya aina hiyo kutokea tena.