Try Again: Simba Itaitikisa Afrika



Try Again: Simba Itaitikisa Afrika
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try again’, amesema mipango ya Simba kwa sasa ni kutawala soka la Afrika na kutetea ubingwa.

Try Again alifunguka kuwa timu hiyo kwa sasa ina mwenendo mzuri baada ya mechi chache na mambo yanavyokwenda atakuja kuonekana mrithi sahihi wa Luis Miquissone kutokana na kuimarika kwa wachezaji kadhaa kwenye timu hiyo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Try Again alieleza kuwa wanataka kulishika soka la Afrika na ndiyo maana wamekuwa makini sana kwenye kutafuta wachezaji ambao wataitumikia timu hiyo kwa sasa na dalili za sasa zinaonyesha kuwa wanakwenda kulitimiza hilo.

“Tunakwenda kuliteka soka la Afrika, hiyo ndiyo mipango yetu, timu sasa imeanza kuimarika na kuna wachezaji nyota wameanza kuonyesha kuwa wao ni wa levo nyingine kabisa, tutawaona kina Miquissone wapya muda siyo mrefu.


 
“Tupo makini kwenye kufanya usajili lengo kubwa ni kuwa na timu imara zaidi itakayotikisa kwenye levo za kimataifa,” alisema Try Again.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad