“Nimekua bibi harusi kwa mara ya kwanza nikiwa na miaka 61, baba yangu mwenye miaka 88 alinipeleka kanisani na kunikabidhi kwa mume wangu” Akiongea sentensi hiyo kudhihirisha kuwa hakuna mwisho wa kupata mapenzi ya dhati, Alice Lewes amekua bibi harusi kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 61.
Kumshika baba yangu mkono na kuingia nae kanisani nikiwa nimevaa shela, sikuweza kuacha kutabasamu, kwanza sidhani kama ningekua na njia nyingine zaidi ya kutabasamu wakati wote.
Alice Lewes mkazi wa London uingereza, anasimulia kisa chake cha mapenzi kuanzia alipokua mtoto mpaka umri huu anaoolewa akisema hakuwahi kufikiria kuvaa gauni jeupe kama bibi harusi.
“Nimezaliwa na kukua Cardiganshire huko Wales, na katika miaka yangu ya 20 nilikua nafanya kazi ya kulea watoto kwenye nyumba za watu huko London. Nilipenda sana watoto lakini niliwachoka nilipofanya kazi hizo kwa muda mrefu hivyo sikuhisi kama uhalisia wangu unanihitaji kuwa na mtoto wa kumzaa na kuwa na maisha yangu.” Alisema Alice.
“Nimekua katika mahusiano ya mapenzi kwa miaka mingi, lakini nilipoona marafiki wanapeana talaka nilishindwa kujua kama ndoa ni jambo zuri au ni laana ya kujiingiza mwenyewe”.
“Ilipofika Juni 2003, rafiki yangu alinialika nyumbani kwake kwa sherehe, wakati huo nina miaka 45, nikiwa namiliki biashara, nafundisha shule za uongozi, na nilikua na furaha kwa namna ya maisha yangu. Lakini aliponiomba aniunganishe na mkulima alietalakiana na mke wake, nilikubali, sikuona tatizo.”
Alice anasema Mwanaume huyo alikua na miaka 54, ni kama kituko lakini siku hiyo ilikwenda vizuri huku wakifurahi kucheza na kupiga hadithi mbalimbali ingawa hapakuwa na hisia yoyote ya kimapenzi, baada ya wiki mbili walikutana tena. “hpo nilihisi kitu mwilini mwangu.” aliongeza Alice.
“Tulianza mahusiano kupata busu la kwanza, tuliendelea kwa kutembeleana na kutoka na marafiki, nyakati nyingi za jioni tulikua na matembezi ya pamoja. Mpaka ilipofika ‘boxing day’ 2006, Johnny alinivalisha pete ya uchumba ya chuma, kwa mshtuko nilitetemeka kwa sababu sijawahi kuhisi hatua kama hiyo maishani mwangu, nilikubali na tukawa wachumba rasmi,” Alice alisimulia.
“Mama yangu alifariki mwaka 1993, akiwa na miaka 57 lakini baba yangu na bibi yangu walikuwepo siku hiyo na walishtushwa, lakini baadae tulibadilisha pete hiyo ya chuma na pete nyingine nzuri ya vito vya thamani ambayo nilipewa na bibi yangu.”
Mimi na Johnny tulifurahia kuwa kwenye uchumba lakini hatukuwa na mpango wa kufunga ndoa. Watu wengi walishangaa na kuona sio jambo la kawaida lakini sisi hatukuona shida hasa pale ambapo mimi niliishi London na Johnny aliishi Essex, tuliendelea kutembeleana na kuonana kila tulipohitajiana.
Miaka 12 baadae tulipokua nyumbani kwetu Wales kwa ajili ya krismasi tukaamua ni wakati sahihi wa kufanya hatua inayofuata ambayo ni ndoa, wakati huo nina miaka 60 na niliona ndio wakati sahihi wa kuolewa.
Mnapokua vijana mnapata mihemko ya ndoa na sherehe kubwa ila sisi tuliamua shrehe ndogo itakayokua na watu wa familia, tulichagua ukumbi karibu na nyumbani kwao Johnny, gauni langu la harusi sikuhangaika niliita fundi akanipima akanishonea linalofika magotini ila jeupe.
Marafiki zangu walinichukua na kunifanyia sherehe ndogo huko urafansa na wote tulikua ni watu wa miaka 60 wakiwemo wanaume, hiyo ilikua kwa upande wangu lakini kwa upande wa Johnny hakufaya sherehe yoyote kwa sababuhakua mpenzi wa sherehe.
Sherehe yangu haikua na waalikwa wala music mkubwa inagwa kulikua na vyakula na vinywaji vya kulevya kiasi kwamba rafiki yangu mmoja alianguka juu ya meza aliyokua akicheza baada ya kulewa.
Siku ya harusi sikuwa najiskia kuogopa wakati najiandaa ila ilipofika wakati wa kuingia kanisani nilihisi mwili unatetemeka, baba yangu alikua amevaa suti iliyoondoa uzee wake na alinikabidhi kwa Johnny.
Baada ya ndoa kuisha na sherehe kumaliziaka sasa ulikuwa wakati wetu kunywa na kufurahia usiku wa ndoa yetu, baada ya hapo ndipo tukaanza kuishi pamoja ambapo Johnny amekua akishikwa sana na vipindi hivi vya Corona.
Alice anamalizia kwa kusema “kuolewa na Johnny imekua jambo jema kwenye maisha yangu kwa sababu ndoa inasaidia kwenye urasimu wa maisha na maswala yote ya kisheria kadri umri unavyokua mkubwa, lakini kikubwa zaidi ni kupata rafiki bora ambae kila wakati unakua unahitaji kukaa nae na kuzungumza na kuwa na furaha,” alimalizia Alice