Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA,) imetoa tahadhari ya upepo mkali leo January 25,2022 unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 katika baadhi ya meneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi (Mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es salaam na Pwani), ikijumuisha Visiwa vya Mafia pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba).
Kimbunga Kenneth: Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania yathibitisha ujio wa upepo mkali - BBC News Swahili
Mamlaka imetoa angalizo kwa wanaofanya shughuli za uvuvi, nyumba zenye mapaa yasiyo imara na wananchi kutokaa chini ya miti ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na upepo huo.